Vigezo na Masharti
Tafadhali soma kwa makini Vigezo na Masharti haya kabla ya kutumia tovuti na huduma za Makazi Solutions (T) Limited.
Tafadhali soma kwa makini Vigezo na Masharti haya kabla ya kutumia tovuti na huduma za Makazi Solutions (T) Limited.
Imesasishwa: Julai 2026
Kwa kufikia au kutumia tovuti hii, unakubaliana na Vigezo na Masharti haya pamoja na taratibu zinazohusiana na huduma za Makazi Solutions (T) Limited. Ikiwa hukubaliani na masharti haya, tafadhali acha kutumia tovuti hii.
Kuweka booking ya kiwanja hakumaanishi kwamba umiliki wa kiwanja umekamilika. Booking ya Tsh 20,000 hutumika kuhifadhi kiwanja ulichochagua wakati unakamilisha taratibu zinazohitajika. Umiliki wa kiwanja unategemea upatikanaji wa kiwanja, kukamilika kwa taratibu za mauzo, malipo yanayohitajika na nyaraka husika.
Taarifa kuhusu miradi, viwanja, bei, upatikanaji, ukubwa na vipengele vingine vya mradi zinaweza kubadilika kulingana na hali ya mradi na taarifa mpya zinazotolewa na kampuni. Kwa taarifa za sasa kuhusu viwanja vinavyopatikana, bei na taratibu za ununuzi, tafadhali wasiliana na Makazi Solutions (T) Limited.
Maudhui yote yaliyopo kwenye tovuti hii, ikiwa ni pamoja na maandishi, picha, nembo, michoro, ramani, video, nyaraka na miundo ya tovuti, ni mali ya Makazi Solutions (T) Limited isipokuwa pale ambapo imeelezwa vinginevyo. Maudhui hayo hayapaswi kutumiwa, kunakiliwa au kusambazwa bila ruhusa inayofaa.
Makazi Solutions (T) Limited hujitahidi kuhakikisha kuwa taarifa zinazowekwa kwenye tovuti ni sahihi na zinaendana na taarifa za kampuni na miradi yake. Hata hivyo, taarifa kama bei, upatikanaji wa viwanja na maendeleo ya miradi zinaweza kubadilika. Kwa taarifa ya mwisho na sahihi, mteja anashauriwa kuwasiliana moja kwa moja na kampuni.
Tovuti hii inaweza kuwa na viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au huduma za watu au taasisi nyingine. Makazi Solutions (T) Limited haiwajibiki moja kwa moja kwa maudhui, huduma au sera za tovuti hizo za nje.
Masharti haya yatazingatia na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria zinazotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makazi Solutions (T) Limited inaweza kufanya marekebisho ya Vigezo na Masharti haya pale inapohitajika. Toleo lililosasishwa litawekwa kwenye ukurasa huu ili watumiaji waweze kupata taarifa za sasa.
Kwa maswali au maelezo zaidi kuhusu Vigezo na Masharti haya, wasiliana na Makazi Solutions (T) Limited kupitia: